Taifa Gas kwa kushirikiana na Benki ya Nmb Tumeendelea na Programu Maalumu ya kijiji day Ambapo Tutatembelea vijiji mbalimbali na kutoa Elimu ya gas Ikiwa ni Jitihada za kuunga mkono Serikali Katika kuhamasisha Jamii hasa Zinazopatikana pembezoni kuacha matumizi ya kuni na mkaa na kuhamia kwenye nishati safi.
hapa ni Katika eneo la Msowero vijijini Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro Ambapo Baada ya Kutoa Elimu na Wananchi Kuwa na Mwitikio Chanya Kampuni yetu Imeweza kuuza mitungi 129.

Aidha Hafla hiyo ilihudhuliwa na Mkuu wa wilaya hiyo Mhe. Hamduni Shaka.