Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Taifa gas katika juhudi za kumuunga mkono Dkt Samia Suluhu Hassan katika jitihada zake za kupambana na mazingira kupitia nishati safi ya kupikia kampuni ya Taifa gas imekabidhi mitungi 300 ya gesi kwa wafanyabiashara katika soko la Samaki ferry jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Ferry Meneja ]Maasoko na Uhusiano wa Taifa gas, Bw Oscar Shelukindo alisema kwamba siku hii ni muhimu kwa sababu kuna mkutano mkubwa wa kimataifa wa nishati nchini unaendelea wenye kutoa mustakabali wa kijani kibichi na endelevu hapa nchini.

“Jitihada hizi ni kuhakikisha kwamba mapinduzi ya kijani yanafanikiwa kwa watanzania wengi zaidi kuanza kutumia nishati safi kwa ajili ya kupikia ili kuchochea ukuaji wa biashara zao na Uchumi kwa ujumla,” alisema shelukindo

Alisema kwamba dhamira ya Taifa gas ni kuunga mkono agenda ya nishati safi inayoongozwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan juhudi hizo zinaenda na uongozi wake wenye maono na kujitolea kwa mheshimiwa Rais katika mandhari nzima ya nishati safi nchini.

“Leo, tunakabidhi mitungi 300 ya gesi, mitungi 100 ya kilo 38 na 200 ya kilo 6 kwa wafanyabiashara (wanaokaanga Samaki) hapa Ferry, ishara ya kuendeleza suluhisho la nishati safi kwa wote,” alisisitiza.

Aliongeza kwamba juhudi hizo inawakilisha matamanio yao ya Pamoja ya kupunguza utegemezi wa kuni na mkaa yanayoharibu mazingira na kwa kutoa mitungi hiyo ya nishati safi, wanaalenga kuboresha maisha ya jamii ya watanzania hususan wapishi wa ferry na kukuza afya na usalama, na kulinda mazingira kwa manufaa ya vizazi vijavyo.

Bw Shelukindo alisema kwa pamoja, wanaweza kufikia malengo yao na kuhakikisha Tanzania inaendelea kua kinara katika maendeleo endelevu ya matumizi ya nishati safi duniani.